Hezbollah na Hamas wamekutana Beirut kujadili upinzani dhidi ya Israel

Ismaïl Haniyeh, mkuu wa vuguvugu la Palestinian Islamist la Hamas

Ismail Haniyeh mkuu wa vuguvugu la Palestinian Islamist la Hamas linalotawala ukanda wa Gaza yupo katika mji mkuu wa Lebanon tangu Jumatano. Israel inalaumu Hamas kurusha roketi 34 kuelekea eneo lake kutoka kusini mwa Lebanon ngome ya vuguvugu la Kishia linaloungwa mkono na Iran, la Hezbollah

Viongozi wa makundi yenye silaha ya Hezbollah na Hamas wamekutana mjini Beirut kujadili utayari wa kuhimili upinzani dhidi ya Israel taarifa ya Hezbollah imesema Jumapili.

Ismail Haniyeh, mkuu wa vuguvugu la Palestinian Islamist la Hamas ambalo linatawala Ukanda wa Gaza amekuwa katika mji mkuu wa Lebanon tangu Jumatano. Israel ilililaumu kundi la Hamas kwa kurusha roketi 34 siku iliyofuata kuelekea eneo lake kutoka kusini mwa Lebanon ngome ya vuguvugu la Kishia linaloungwa mkono na Iran la Hezbollah.

Jeshi la Israel lililipiza kisasi Ijumaa kwa mashambulizi kusini mwa Lebanon na Gaza baada ya roketi kuilenga Israel ambazo pia zilirushwa kutoka eneo la pwani. Wakati wa mkutano wa Haniyeh na mkuu wa Hezbollah Hassan Nasrallah wawili hao pia walijadili utayari wa kuhimili wa upinzani na ushirikiano kati ya wanachama wake kutokana na matokeo ya karibuni taarifa ya Hezbollah ilisema.

Mhimili wa upinzani unazelezewa kuwa ni Lebanon, Palestina, Syria na makundi mengine yanayoungwa mkono na Iran yanayoipinga Israel. Wawili hao pia walijadili kuongezeka kwa upinzani huko Ukingo wa Magharibi na Gaza na matukio kwenye msikiti wa Al-Aqsa mjini Jerusalem kulingana na taarifa hiyo ambayo haikufafanua walipokutana.