Walinzi wa bahari wa Japan wanaendelea na operesheni ya kutafuta na kuokoa ndege ya helikopta ya kijeshi iliyotoweka kwenye mitambo Alhamisi karibu na visiwa vya kusini magharibi karibu na Taiwan.
Yasunori Morishita, ambaye ni kiongozi wa vikosi vya kijeshi vya ardhini vya Japan, GSDF wakati akizungumza na wanahabari Alhamisi amesema kwamba helikopta hiyo aina ya Black Hawk inaaminika kuanguka baharini kufuatia kuonekana kwa vifusi vinanyofanana na vya ndege karibu na eneo hilo.
Maafisa wa GSDF wamesema kwamba helikopta hiyo ilikuwa imebeba watu 10, wakati ikifanya uangalizi karibu na kisiwa cha Miyakojima, takriban 400 mashariki mwa Taiwan. Ndege hiyo ilitoweka Alhamisi kwenye mtambo wa mawasiliano wa radar saa kumi na dakika 33 jioni saa za huko.
Meli za ulinzi za kijeshi za Japan tayari zimetumwa kujiunga na GSDF kwenye eneo la tukio ili kusaidia kwenye operesheni za uokozi.