Nasrin Sotoudeh mwenye umri wa miaka 60 alikamatwa Jumapili kwenye mazishi ya msichana Armita Garawand mwenye umri wa miaka 17, ambaye kifo chake kilitangazwa na chombo cha habari cha serikali, baada ya kupoteza fahamu kwa mwezi mmoja.
Tukio hilo lililofanyika Oktoba mosi limeibua kisa cha Mahsa Amini msichana aliyekufa akiwa mikononi mwa polisi Septemba mwaka jana, baada ya kuzuiliwa kwa madai ya kutovaa hijabu, wakati mamlaka zikijitahidi kuzuia maandamano sawa na yaliyofuatia kifo chake.
Wakili Sotoudeh ambaye ndani ya muongo mmoja uliyopita amekuwa nje na ndani ya jela kufuatia kesi kadhaa kutokana na uanaharakati wake, muda mfupi baada ya kukamatwa alipelekwa kwenye jela ya wanawake ya Qarchak,iliyopo nje ya Tehran, kulingana na ujumbe wa Facebook kutoka kwa bwanake Reza Khandan.