“ Juhudi zinazokinzana hazisaidii na zinaongeza migawanyiko iliyopo nchini, huku zikihujumu juhudi za ukarabati, kinyume na uungaji mkono na umoja wa kitaifa ulioonyeshwa na watu wa Libya,” amesema kupitia taarifa.
Libya imekuwa na serikali dhaifu tangu 2011 kufutia mapinduzi yaliongozwa na NATO, lakini ikagawanyika tena 2014 kati ya serikali iliyopo magharibi na nyingine upande wa mashariki. Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters serikali ya mashariki ilisema kwamba imeahirisha kongamano na kimataifa lililokuwa lijadili ukarabati wa Derna.
Serikali inayotambuliwa kimataifa yenye makao yake makuu mjini Tripoli upande wa magharibi ilisema pia ilikuwa ikipanga mkutano wa kujadili kuhusu ukarabati wa Derna. Wachambuzi wanasema kwamba ukarabati wa Derna unaotarajiwa kuleta fedha nyingi kutoka mataifa ya kigeni huenda ukasababisha ghasia mpya kati ta serikali zote mbili.