Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres ametoa wito siku ya Jumatano kwa Israel na Hamas kuongeza muda wa sitisho la mapigano kwa muda, akisema “makubaliano ya kweli ya sitisho la kibinadamu” yanahitajika katika vita vilivyodumu kwa wiki nane.
“Watu wa Gaza wako kati-kati ya janga kubwa la kibinadamu mbele ya macho ya ulimwengu”, Antonio Guterres ameuambia mkutano wa ngazi ya mawaziri wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu hali hiyo. “Hatupaswi kuangalia pembeni”. Alifuahishwa na malori kadhaa ya misaada kwa kupeleka mafuta ambayo yameingia Gaza, kote kusini na kaskazini wakati wa sitisho a muda lilipoanza Ijumaa.
Tangu wakati huo, mateka 60 waliokuwa wakishikiliwa na Hamas na wafungwa 180 wa Kipalestina pia wameachiliwa huru. Lakini Guterres amesema “masuala mengi zaidi” yanahitajika kushughulikia mahitaji ya kibinadamu ya wakaazi milioni 2.2 wa Gaza.
Aliisihi Israel kufungua vivuko zaidi vya mpakani, ambavyo vipi hivi sasa na kutaka kwa sekta binafsi kuanza tena shughuli za kibiashara.