Giuliani awasilisha kesi ya kufilisika huku akitakiwa kulipa karibu dola milioni 150

Rudy Giuliani, mwanasheria wa zamani wa kampeni ya Trump

Kufunguliwa kwa kesi hiyo kunafuatia uamuzi wa jaji wa serikali kuu siku ya Jumatano kwamba Giuliani lazima amlipe mara moja Wandrea “Shaye” Moss na Ruby Freeman, kwa kueneza madai yasiyo na msingi juu ya kuhusika kwao katika udanganyifu wa uchaguzi

Mwanasheria wa zamani wa kampeni ya Trump, Rudy Giuliani amewasilisha kesi ya kufilisika, siku moja baada ya jaji wa serikali kuu kuamuru alipe mara moja takribani dola milioni 150 kwa wafanyakazi wawili wa zamani wa uchaguzi wa jimbo la Georgia kutokana na kashfa.

VOA Kumekucha Afrika imezungumza na mchambuzi wa siasa za Marekani, Timothy Sadera kutoka jimbo la Georgia nchini Marekani na kwanza kutaka kujua hatua hii aliyochukua Giuliani ina maanisha nini.

Your browser doesn’t support HTML5

Mahojiano na mchambuzi wa siasa Timoth Sadera akiwa Georgia, Marekani.m4a

Katika jalada la kufilisika la Sura ya 11, lililowasilishwa Alhamisi huko New York, Giuliani aliripoti mamilioni ya dola katika deni kutoka kwa mashtaka, kodi zisizolipwa na ada za kisheria.

Kufunguliwa kwa kesi hiyo kunafuatia uamuzi wa jaji wa serikali kuu siku ya Jumatano kwamba Giuliani lazima amlipe mara moja Wandrea “Shaye” Moss na Ruby Freeman, kwa kueneza madai yasiyo na msingi juu ya kuhusika kwao katika udanganyifu wa uchaguzi.