Ghasia zaripotiwa katika sehemu nyingi za Nigeria wakati wa uchaguzi wa rais na bunge

Watu wakisubiri kupiga kura Nigeria

Mashambulizi na ghasia zimeripotiwa kote nchini Nigeria wakati raia walipokwenda kupiga kura kumchagua rais na viongozi wengine, licha ya mamlaka kupeleka vikosi vizito vya usalama . Nigeria yenye idadi kubwa ya watu barani Afrika imekuwa ikijitahidi kutokomeza ghasia na kuboresha uchumi wake.

Wapiga kura waliwasili katika vituo vya kura katika wilaya ya Apo mjini Abuja mapema Jumamosi lakini walisema iliichukua muda kabla ya maafisa wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi kuwasili na kufungua vituo. Mchakato huo unafuatiliwa na timu za maafisa wa usalama, likiwemo jeshi, polisi na vikosi vya kiraia.

Nigeria inachagua rais mpya na makamu rais, maseneta na wawakilishi wa bunge katika uchaguzi ambao unajumuisha wapiga kura milioni 93. Nigeria pia inakabiliwa na matatizo ya kiuchumi. Matumizi ya serikali na madeni yamekuwa yakiongezeka, kuongeza wasi wasi kuhusu uwezo wa Nigeria kulipa madeni yake.

Mpiga kura atumbukiza vyeti vya kura yake kwenye sanduku mjini Agulu, Nigeria

Benki Kuu inatekeleza sera ya mageuzi ya sarafu ambayo yamepelekea uhaba wa Naira ya Nigeria, na kusababisha maandamano mabaya na kuumiza uchumi wa nchi.

Ijumaa, maafisa wa usalama walikamata kiasi cha dola 500,000 taslimu kutoka kwa mbunge wa baraza la wawakilishi wa jimbo la Rivers, saa kadhaa baada ya idara ya kupambana na rushwa kuingilia kati na kukamata dola 70,000 zinazoshukiwa kuwa ni za kununua kura mjini Lagos.

Matatizo ya ukosefu wa usalama na uchumi yalikuwa masuala makuu wakati wa kampeni. Nigeria inajitahidi kudhibiti kusambaa kwa ghasia, ikiwemo uanamgambo wa kiislamu, utekaji nyara na .
wanaotaka kujitenga.

Umamosi, mkuu wa INEC Mahmood Yakubu aliwaelezea waandishi wa habari baada ya ripoti za kuvurugika kwa uchaguzi, ununuzi wa kura na mashambulizi katika baadhi ya majimbo ikiwemo Lagos, Borno na Rivers.

“Tunafuatilia changamoto ambazo tunazo katika maeneo mawili katika jimbo la Borno, baadhi ya majambazi au waasi walikuwa wakifyatua kutoka juu yam lima huko Gwoza, licha ya kufyatua kiholele. Hicho ndiyo tulikuwa tunakifuatilia kabla ya kukutana na nyinyi,” alisema Yakubu.

Nigeria pia inakabiliwa na matatizo ya kiuchumi. Matumizi ya serikali na madeni yamekuwa yakiongezeka, kuongeza wasi wasi kuhusu uwezo wa Nigeria kulipa madeni yake.


Benki Kuu inatekeleza sera ya mageuzi ya sarafu ambayo yamepelekea uhaba wa Naira ya Nigeria, na kusababisha maandamano mabaya na kuumiza uchumi wa nchi.

Wakaazi wa Abuja wako hapa kupiga kura zao. “Usalama ni duni, na uchumi uko chini sana. Nadhani hicho ndiyo kitu kimoja ambacho kinawafanya watu kutoka nje kwa idadi kubwa kupiga kura wakati huu,” alisema Chibueze Onyema mkaazi wa Abuja.


Mkaazi mwingine Musa Sarki kutoka Wilaya wa Apo anasema “Uchaguzi ni huru, changamoto tuliyonayo ni kwamba vifaa vimechelewa kufika. Pili, maafisa hawajipanga, msongamano ni mkubwa sana hapa, ni zaidi ya watu 2,000 wako hapa na wao wamefika saa tatu na nusu.”

Wagombea 18 wako katika ushindani wa urais, lakini watatu ndiyo wanapewa nafasi ya juu. Uchaguzi unaonekana kuwa ni wa wazi sana tangu mwaka 1999, wakati Nigeria ilipotoka kwenye utawala wa kijeshi na kuingia katika utawala wa kidemokrasia.

Ijumaa, mamlaka zilikamata fedha taslimu dola 500,000 kutoka kwa mbunge wa baraza la wawakilishi katika jimbo la Rivers, saa kadhaa baada ya idara ya kupambana na rushwa kuingilia kati na kukamata dola 70,000 zinazoshukiwa kuwa ni kununua kura huko Lagos.