Gavana Joho atembelea Sauti ya Amerika

Studio 15 wakati wa Live Talk pamoja na Ali Hassan Joho Gavana wa Mombasa

Gavana Ali Hassan Joho wa County ya Mombasa huko Kenya , ametoa wito kwa Wakenya wanaoishi nchi za nje warudi nyumbani na kuekeza katika county, na kwamba kuna sheria na kanuni za kurahisisha uwekezaji.

Anasema "Lengo letu kubwa kutembelea Marekani ni kuwatafuta wawekezaji waje Mombasa kuleta mabadiliko kutoka uchumi wa huduma kuelekea uchumi wa uzalishaji na kiviwanda"

Your browser doesn’t support HTML5

Live Talk: Mazungumzo na Gavana Joho


Akiwa katika ziara ya wiki Moja Marekani Bw Joho alitembelea Sauti ya Amerika na kushiriki katika makala ya Live Talk ambapo alijibu maswali ya wasikilizaji juu ya mabo mbali mbali ya utawala, haki za binadam, ulaji rushwa, uwekezaji na usalama.

Seneta wa Mombasa Omar Hassan aliyefuatana na Gavana alikosoa vikali msako uanoendelea kuwasaka magaidi wa kundi la Al-Shabab. Anasema "msako huo hauambatani na maslahi ya kikatiba na inakiuka haki za kibinadam. Na kwamba tumewarudisha wenzetu wa Kisomali katika karne zilizopita, kwamba tumewadhulumu kihalaiki, kwa shutma kwamba tunawatafuta magaidi."