Kwa mujibu wa shirika la habari la AP, shirika hilo kwa jina GiveDirectly, liligundua kuwa baadhi ya wafanyakazi wake nchini Congo walishirikiana na watu wa nje kuvuja fedha zilizolenga kusaidia zaidi ya familia masikini 1,700 ndani ya kipindi cha miezi 6 kuanzia Agosti 2022.
Taarifa zimeongeza kusema kwamba fedha hizo zilipotea baada ya kubadili mfumo wa ulipaji, ili kufikia vijiji vilivyokuwa maeneo ya ndani yasio kuwa na usalama.
Shirika hilo limeongeza kusema kwamba uchunguzi unaendelea ambapo sehemu ndogo ya fedha zilizo ibwa imepatikana, ingawa huenda nyingi zisipatikane. Hata hivyo wameongeza kusema watahakikisha kuwa familia ziliazoathiriwa zitapata misaada yao licha ya wizi huo.