Hilo lilikuwa ni kuhusu uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika Decemba 2O, ukisema kwamba hautaweza kutuma watu kote nchini humo kutokana na sababu za kiusalama. Kupitia taarifa EU imesema, “Kutokana na sababu za kiufundi zilizoko nje ya uwezo wetu, tumefuta upelekaji wa tume ya waangalizi wa uchaguzi huko DRC, kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Jumatano, shirika la habari la Reuters limeripoti.
EU ilikuwa imepanga kutuma waangalizi wake kwenye majimbo mengi ya DRC, lakini sasa hilo halitowezekana. Msemaji wa EU Nabila Massrali mapema wiki hii aliambia Reuters kwamba waangalizi wa EU tayari walikuwa Kinshasa, na kwamba walikuwa waende kote nchini hapo Novemba 21, lakini hilo halikuwezekana kutokana na sababu za kiusalama.
Hali ya taharuki imeendelea kuongezeka nchini humo kuelekea kwenye uchaguzi wa rais na bunge, wakati taifa hilo la pili kwa ukubwa barani Afrika likikabiliana na makundi yenye silaha upande wa mashariki wenye utajiri mkubwa wa madini.