Ethiopia imefungua soko lake la hisa baada ya kukosekana kwa miaka 50

Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed (wa tatu upande wa kulia) akigonga kengele wakati wa uzinduzi wa soko la hisa. Addis Ababa, Ethiopia. January 10, 2025.

"Wekeza nchini Ethiopia, uchumi unakua kwa kasi wenye uwezo mkubwa na njia yenye nguvu kuelekea ustawi" anasema Abiy.

Ethiopia ilifungua soko lake la hisa, Ethiopian Securities Exchange (ESX), siku ya Ijumaa baada ya kukosekana kwa miaka 50. Shughuli za Ethiopian Securities Exchange zilisimamishwa mwaka 1974 kufuatia uongozi kuchukuliwa na serikali ya kijeshi ya kikomunisti.

Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed alielezea uzinduzi huo wa Ijumaa ni “hatua ya kihistoria” kwa uchumi na fedha kwa hali ya Ethiopia. Tumepiga rasmi kengele ya kufungua Ethiopian Securities Exchange, soko la kwanza la hisa kwa nchi yetu.

"Wekeza nchini Ethiopia, uchumi unakua kwa kasi wenye uwezo mkubwa na njia yenye nguvu kuelekea ustawi", aliandika Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed kwenye mtandao wa X.