Ethiopia imefanya mazungumzo ya ushirikiano wa kijeshi na Somaliland

Utiaji saini wa mkataba wa maelewano (MOA) kati ya Ethiopia and Somaliland uliofanyika Addis Ababa.

Mazungumzo hayo yaliyofanyika mjini Addis Ababa yalifanyika siku hiyo hiyo Rais Hassan Sheikh Mohamud wa Somalia ameanza ziara katika nchi jirani ya Eritrea

Ethiopia imesema imefanya mazungumzo Jumatatu juu ya ushirikiano wa kijeshi na Somaliland, wiki moja tu baada ya makubaliano na mkoa uliojitenga na Somalia kuhusu upatikanaji fursa ya baharini na kusababisha mivutano katika Pembe ya Afrika.

Mazungumzo hayo yaliyofanyika mjini Addis Ababa yalifanyika siku hiyo hiyo, Rais Hassan Sheikh Mohamud wa Somalia ameanza ziara katika nchi jirani ya Eritrea. Somalia inatafuta uungwaji mkono wa kimataifa kuhusiana na makubaliano tata ya Januari mosi kati ya Ethiopia na Somaliland mkoa uliojitenga ambao Mogadishu una mamlaka kidogo ya kweli.

Serikali kuu imeutaja mkataba wa maelewano (MOU) ambao unaipa Ethiopia fursa ya kuingia katika Bahari ya Sham kupitia Somaliland, kitendo cha ukandamizaji na ukiukaji wa uhuru wake.