Shirika la ndege la Emirates lenye makao yake Dubai limesema litasitisha safari zake za ndege nchini Nigeria kuanzia Septemba kwa sababu limeshindwa kupata fedha zake kutoka Nigeria.
Tatizo limezuka kwa sababu Nigeria imezuiya kupatikana kwa mabadilishano ya fedha za kigeni, shirika la habari la Reuters limeripoti. Katika taarifa yake Emirates imesema imefanya utaratibu rafiki wa kuwa na majadiliano na maafisa ili kuingilia kati haraka kupata msaada wa utatuzi wa suala hilo, lakini imesema inasikitishwa kwamba hakuna suluhu yoyote iliyopatikana.
Safari za ndege zitasitishwa kuanzia Septemba mosi ili kuepuka gharama zaidi za operesheni. mwezi Juni jumuiya ya kimataifa ya safari za anga ilisema kwamba Nigeria haikutoa dola milioni 450 inayodaiwa na mashirika kadhaa ya ndege, Reuters imeripoti.
Hata hivyo Emirates imeripoti kwamba itazingatia uamuzi wake kama hakutakuwa na maendeleo yoyote chanya katika siku zijazo. Wasafiri walioathiriwa na uamuzi huu wanaweza kurejeshewa fedha zao za tiketi.