Dozi mbili za Pfizer zimeonekana kutoa kinga ya asilimia 70 dhidi ya kulazwa hospitali-Utafiti

Mfanyakazi wa afya akitoa chanjo ya Pfizer kwa mtu mmoja mjini Johannesburg, Afrika Kusini Desemba 9, 2021.

Dozi mbili za chanjo ya Pfizer-BioNTech ya COVID-19 imeonekana kutoa kinga ya asilimia 70 dhidi ya kulazwa hospitali nchini Afrika Kusini katika wiki za karibuni, utafiti mkubwa wa ulimwengu juu ya athari zinazowezekana kutokana na Omicron ulionyesha.

Dozi mbili za chanjo ya Pfizer-BioNTech ya COVID-19 imeonekana kutoa kinga ya asilimia 70 dhidi ya kulazwa hospitali nchini Afrika Kusini katika wiki za karibuni, utafiti mkubwa wa ulimwengu juu ya athari zinazowezekana kutokana na Omicron ulionyesha Jumanne, wakati nchi hiyo ikipambana na kuongezeka kwa maambukizo.

Utafiti huo uliotolewa na msimamizi mkuu wa bima ya afya ya binafsi nchini Afrika Kusini, Discovery Health, ulitokana na zaidi ya matokeo 211,000 ya watu walioambukizwa COVID-19 kutoka Novemba 15 hadi Desemba 7, watu wapatao 78,000 kati yao walihusishwa na Omicron.

Matokeo hayo ya kesi 78,000 hayajathibitishwa kama ni za Omicron, kumaanisha kwamba utafiti huo hauwezi kutoa matokeo ya kuhitimisha juu ya aina hiyo iliyoitwa ya kutia wasiwasi na Shirika la Afya Ulimwenguni.