Dk. Remmy atutoweka

  • Abdushakur Aboud

Mwanamuziki mashuhuri Tanzania na duniani kote Ramadhan Mtoro Ongala amefariki dunia Jumatatu baada ya kua taabani kwa wiki mbili mjini Dar Es Salaam.

Dk. Remmy kama alivyo kua akijulikana zaidi au Sura Mbaya kama alivyopenda kujulikana, amekua kwa muda mrefu akiugua kutokana na magonjwa kadhaa, ikiwa ni pamoja na kisukari, maradhi ya figo, moyo na shinikizo la damu.

Dk Remmy atakumbukwa sana kutokana na nyimbo zake zilizkua zinazungumzia ukweli wa maisha ya kawaida na kutoogopa kuzungumzia suala lolote linalowakera wananchi wa kawaida.

Miongoni mwa nyimbo zake zinazokumbukwa kabisa na kumpatia umashuhuri wa kimataifa ni siku ya kifo. Hata hivyo wimbo wa 'Mrema' unaozungumzia ulaji rushwa ulipendwa sana na hadi hii leo unamulika ukweli wa mambo.

Mwanazmuziki Dr Remmy alizaliwa mnamo mwaka 1947,katika mji Kisangani lakini na kukulia mjini Bukavu huko Jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo enzi hizo ikijulikana kama Zaire kabla ya kuhamia nchini Tanzania mwaka 1977, ambapo alijiunga na Bendi ya Mjomba wake Mzee Makassy na baadaye alijiunga na Super Matimila na kisha kurejea tena kwa mjomba wake Mzee Makassy kabla ya kuachana na Muziki wa kidunia na kuanza kuimba muziki wa kiroho hadi mauti yalipomkuta usiku wa kuamkia Jumatatu.

Marehemu ameacha mjane na watoto watano.