Darzeni wauawa katika mapambano ya karibuni mkoa wa Amhara- Ethiopia; UN

Ramani ya mikoa ya Amhara and Tigray nchini Ethiopia.

Mkoa wa pili wenye idadi kubwa ya watu nchini Ethiopia umeharibiwa na ghasia kwa miezi kadhaa, huku idadi ya mapambano kati ya jeshi la Ethiopia na kundi la wanamgambo wa Amhara linalojulikana kama Fano yameripotiwa katika wiki za karibuni

Umoja wa Mataifa umesema kwamba takriban raia 50 wameuawa katika mapambano na mashabulizi nchini Ethiopia katika mkoa wa Amhara katika muda wa mwezi mmoja uliopita.

Mkoa wa pili wenye idadi kubwa ya watu nchini Ethiopia umeharibiwa na ghasia kwa miezi kadhaa, huku idadi ya mapambano kati ya jeshi la Ethiopia na kundi la wanamgambo wa Amhara linalojulikana kama Fano yameripotiwa katika wiki za karibuni.

“Ni muhimu kwamba pande zote zijizuie kutokana na mashambulizi ya kinyume cha sheria na kuchukua hatua zote muhimu kuwalinda raia,” Seif Magango, msemaji wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya haki za binadamu amesema katika taarifa yake.

Alielezea wasi wasi wake mkuu katika “athari za kusikitisha za mashambulizi ya ndege zisizotumia rubani-drone na ghasia nyingine kwa watu katika mkoa wa Amhara” huku mapambano yakiendelea.

Takriban watu 47 wameuawa katika mashambulizi matano tofauti tangu mwanzoni mwa Oktoba, amesema.

“Wote walikuwa raia,” aliliambia shirika la habari la AFP.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Antony Blinken alielezea wasi wasi wake kuhusu ghasia alipozungumza kwa simu na Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed.

Blinken “alisisitiza umuhimu wa majadiliano na mashauriano katika kusuluhisha mzozo,” msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje, Mathew Miller amesema.

Kwa suala tofauti alimpongeza Abiy kwa kuruhusu mageuzi ya kufuatilia ambayo imeitia moyo Marekani kuanza tena kutuma msaada wa chakula nchini Ethiopia, ambayo inatoka kwenye vita vya umwagaji damu vya miaka miwili katika mkoa wa Tigray.

Shirika la Marekani la Kimataifa la Maendeleo limesitisha misaada mwezi Juni, likidai kampeni ya kimfumo kubadili mwelekeo wa misaada ya chakula.

Kuikamata tena Lalibela

Wiki iliyopita, jeshi la Ethiopia lilipata tena udhibiti wa Lalibela- Kituo cha Urithi cha UNESCO ambacho kimekuwa kikijulikana kwa karne nyingi ambako kuna makanisa, baada ya wanamgambo wa mkoa huo Fano kuuvamia mji wa kihistoria siku mbili kabla.

Kumekuwepo na idadi ya vifo isiyo rasmi kutokana na mapigano ya Novemba 8, lakini mkuu wa kanisa alisema alihudhuria mazishi siku iliyofuata ya maafisa polisi 16 waliouawa katika mapambano. Mkuu wa kanisa aliongeza kwamba alifahamu kuhusu raia mmoja aliyefariki na mwanamke ambaye alijeruhwia.

Magango hakuweza kutoa idadi ya vifo kutokana na mapambano lakini amesema shambulizi la drone ambalo lilipiga kituo cha basi huko Wabe hapo Novemba 9 na kuua watu 123 waliokuwa wakisubiri kupanda basi.

“Wanamgambo wa Fano wameripotiwa kufanya harakati zao katika eneo na kushambulia jeshi au kambi wakati shambulizi la drone lilipopiga,” amesema.

Mashambulizi kama hayo ni sawa na kuwanyima maisha watu kwa mujibu wa sheria za kimataifa za haki za binadamu.”

Siku tatu awali, shambulizi la drone linalodaiwa kufanywa na majeshi ya serikali lilipiga shule ya msingi katika wilaya ya Wadera, na kuua watu saba, wakiwemo waalimu watatu, amesema.

Hapo Novemba 4, watu sita waliuawa na 14 kujeruhiwa wakati majeshi ya serikali yalipopiga maeneo ya makazi katika eneo la Central Gondar, amesema.

“Waathirika wengi waliuawa katika nyumba zao.”

Magango amesema watu wengine 21 wakiwemo maafisa wa serikali na chama tawala, waliuawa na wanamgambo wa Fano katika mashambulizi tofauti katika mkoa hapo Oktoba 9 na 28.

Ingawaje Fano wamepigana sambamba na majeshi ya serikali katika vita vya miaka miwili katika nchi jirani katika mkoa wa Tigray, mivutano imezuka baada ya Addis Ababa kutangaza mwezi April kwamba inalivunja jeshi la kimkoa kote nchini Ethiopia.

Serikali ya Ethiopia imeweka hali ya dharura mwezi Agosti baada ya mapigano kuzuka huko Amhara, na kuongeza wasi wasi mpya kuhusu uthabiti wa taifa la pili lenye watu wengi zaidi barani Afrika.