CUF yasema baadhi ya wakazi wa Zanzibar wakimbilia Mombasa

Mashabiki wa chama cha CUF mjini Unguja, Zanzibar

Siku kadhaa kabla ya kufanyika uchaguzi mkuu wa marudio huko Zanzibar, Chama cha Wananchi -CUF kimesema baadhi ya wanachama wake huko kisiwani Pemba wameanza kukimbilia maporini wakitafuta uwezekano wa kutoroka kisiwani humo na kukimbilia katika mji wa Mombasa nchini Kenya ili kutafuta hifadhi ya ukimbizi.

Your browser doesn’t support HTML5

Ripoti ya Munir Zakaria wa Zanzibar

Hatua hii inafuatia madai ya kuwepo kwa taharuki na kamata kamata inayoendelea huko dhidi ya watu wanaodaiwa kuhusika na matukio ya kuchomwa moto kwa baadhi ya nyumba.

Uchaguzi mkuu wa marudio unatokana na kufutwa kwa matokeo ya uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 25 mwaka jana ambao ulisemekana uligubikwa na kasoro.

Wakati huo huo Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar bwana Mohamed Aboud alisema serikali imejipanga vizuri kuhakikisha uchaguzi wa marudio unafanyika katika mazingira ya Amani na utulivu.

Polisi wakipiga doria katikia mitaa ya Zanzibar

Aidha aliwataka wananchi kuondokana na khofu hasa katika kipindi hiki ambacho askari katika jeshi la wananchi wa Tanzania- JWTZ wanaendelea na mazoezi yao ya kawaida ya kila mwaka huko Zanzibar.