Clinton ajibu wakosoaji vikali.

Waziri Clinton akijibu maswali ya wabunge kuhusu Libya.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Hillary Clinton amejitetea vikali kutokana na lawama za jinsi alivyosimamia wizara hiyo wakati wa mashambulizi mabaya ya Septemba 11 katika ubalozi mdogo wa Marekani huko Benghazi ,Libya na kupinga ukosoaji wa baadhi ya wabunge kwamba kulikuwa na jaribio la kuwahadaa wananchi wa Marekani juu ya kile kilichotokea .

Akijitetea vikali waziri Clinton alitoa ushahidi Jumatano mbele ya kamati mbili za bunge zinazochunguza shambulizi hilo ambalo lilimuuwa balozi wa Marekani Christopher Stevens na wamarekani wengine watatu .

Your browser doesn’t support HTML5

Mahojiano na Mitinyi


Clinton aliiambia kamati ya mambo ya nje ya bunge anawajibika kwa mapungufu yaliotokea katika ulinzi kwenye ubalozi mdogo wa Marekani huko Benghazi .

Akitoa majibu katika kikao hicho waziri Clinton alisema kutokuwa na uthabiti huko Mali kunapelekea kuwepo kwa eneo salama la magaidi ambao wanatafuta hifadhi katika maeneo ya kaskazini mwa Afrika.

Aliongeza kuwa Marekani na washirika wake wamekuwa wakifanya kazi na majirani wa Mali ili kuongeza usalama lakini wengi hawana uwezo wa kufanya hivyo.

Maelezo yake yametolewa wakati ongezeko la majeshi ya Ufaransa na Afrika yakiingia Mali kusaidia jeshi la nchi hiyo kuwaondoa wanamgambo wa kiislam kutoka kwenye ngome yao huko kaskazini.