China, Iran na Russia zinajihusisha na uingiliaji kati wa kigeni huko New Zealand, shirika la upelelezi la taifa hilo limesema Ijumaa baada ya kutoa ripoti yake ya tathmini ya vitisho kwa umma, kwa mara ya kwanza.
Katika ripoti hiyo Mkurugenzi Mkuu wa Usalama Andrew Hampton alisema Idara ya huduma za Upelelezi wa Usalama inaona thamani kubwa katika kushirikiana zaidi ufahamu wake kwa umma. Shirika hilo hapo awali lilikuwa limechukua mtazamo wa siri.
Iliamua kubadili mwelekeo baada ya shirika hilo na mashirika mengine kukosolewa kwa kujikita zaidi katika kitisho kinachodhaniwa kutoka kwa itikadi kali za Kiislamu na kutofahamu vyema wakati mzungu mmoja alipowapiga risasi na kuwaua waumini 51 katika misikiti miwili ya Christchurch mwaka 2019.
Katika ripoti hiyo, shirika hilo linasema kuwa kesi zinazofahamika sana za uingiliaji wa kigeni ziliendelea kulenga jamii mbalimbali za China na watu wenye uhusiano na kitengo cha upelelezi cha Chama tawala cha Kikomunisti cha China.