China inaharakisha Kuwachanja watu wake walio mazingira hatarisi leo Alhamisi kwa matarajio ya kupunguza wimbi la maambukizi ya COVID-19 huku baadhi ya wachambuzi wakitarajia Idadi ya vifo kuongezeka baada ya kulegeza msharti makali ya udhibiti uliowekwa awali ili kudhibiti janga hilo kwa miaka mitatu.
Msukumo huo unakuja wakati Shirika la Afya Duniani (WHO) pia likielezea wasiwasi kwamba idadi ya watu bilioni 1.4 nchini China hawakupatiwa Chanjo za kutosha na Marekani ilitoa msaada katika kukabiliana na kuongezeka kwa maambukizi.
Beijing Jumatano iliyopita ilianza kuvunja sera yake ngumu ya udhibiti wa 'ZERO-COVID' kuacha mahitaji ya upimaji na kurahisisha
Sheria za karantini ambazo zilikuwa zimesababisha msongo wa mawazo kwa mamilioni ya watu na kuathiri uchumi wa pili kwa ukubwa duniani.