“Matatizo ya demokrasia yanahitaji kutatuliwa kwa demokrasia zaidi”, alisema Boric akiwa kwenye makao ya rais ya La Modena ambayo yalishambuliwa na ndege za kijeshi mwanzoni mwa mapinduzi hayo miaka 50 iliyopita. “Mapinduzi ya kijeshi au ukiukaji wa haki za binadamu kutoka kwa wale wanaofikiria tofauti hayakubaliki kamwe”, Boric alisema kwenye hotuba yake kwa taifa.
Hata hivyo watu wengi wa Chile wanaamini kwamba mapinduzi ya 1973 yalifaa, na kwamba Pinochet aliyekufa 2006 alikuwa kiongozi mwema aliyeleta maendeleo nchini Chile. Utawa wa Pinochet unafahamika kwa kukiuka haki za binadamu, kuuwa na kufunga wapinzani, pamoja na kutesa maelfu walioukosoa.
Zaidi ya watu 3,200 wanasemekana kuuawa na utawala huo huku wengine 1,469 wakitoweka. Miaka 50 baadaye, watu 297 wamehukumiwa kutokana na ukatili wa kibinadamu, wakati kesi dhidi ya wengine 1,300 zikiwa zinaendelea kusikilizwa.