Chama tawala cha Waziri mkuu wa Cambodia Hun Sen kinadai kuwa kimeshinda kwa kishindo katika uchaguzi mkuu wa Jumapili na kupata karibu viti vyote 125 bungeni.
Uchaguzi haukupingwa na kundi kuu la upinzani wa kisiasa Candlelight Party kwa mujibu wa Sok Eysan, msemaji wa chama tawala cha Cambodian People’s Party au CPP.
Chama cha Sok Esyan kilisema kilishinda kwa kiasi cha kiwango cha asilimia 78 mpaka 80.Tume ya taifa ya uchaguzi ilisema idadi ya watu waliojitokeza kupiga kura ilikuwa asilimia 84 kati ya watu milioni 9.7 waliojiandikisha kupiga kura.
Kiti kimoja au viwili vinaweza kuchukuliwa na vyama vingine Sok Eysan aliiambia VOA. Haya ni mafanikio makubwa na ushindi wa kishindo aliongeza.