Chama cha Umkhonto we Sizwe (MK) cha rais wa zamani wa Afrika Kusini Jacob Zuma kimewasilisha maombi katika mahakama ya katiba kujaribu kuzuia kikao cha kwanza cha Bunge tangu uchaguzi wa mwezi uliopita, kilisema siku ya Jumanne.
Bunge jipya la Afrika Kusini lililochaguliwa hivi karibuni linatarajiwa kukutana siku ya Ijumaa kwa ajili ya kuapishwa kwa wabunge na uchaguzi wa spika na naibu spika pamoja na rais wa nchi.
Chama cha Zuma cha MK kilishangaza kwa kupata nafasi ya tatu katika kura ya Mei 29 lakini kinadai kuwa wizi wa kura ulifanyika na kutishia kususia bunge jipya.
Tume Huru ya Uchaguzi na vyama vingine vilisema uchaguzi ulikuwa huru na wa haki, na Afrika Kusini haina historia ya wizi mkubwa wa kura.