Chad imewakamata watu 80 na kuzuia operesheni za uasi nchini humo

Ramani ya Chad na nchi zilizo jirani nae

DGRM ilisema katika taarifa kundi lililoandaliwa vizuri la watu ndani ya vuguvugu la M3M lilijaribu kuhujumu usalama wa serikali.

Idara ya ujasusi ya jeshi la Chad imesema imewakamata zaidi ya watu 80 na kuzuia operesheni za uasi zinazotishia usalama wa taifa.

“Idara Kuu ya Ujasusi wa Kijeshi (DGRM) ilisema katika taarifa kwamba kundi lililoandaliwa vizuri la watu ndani ya vuguvugu la M3M lilijaribu kuhujumu usalama wa serikali”.

Taarifa hiyo iliyotumwa kwa shirika la habari la AFP na waziri wa mawasiliano, Abderaman Koulamallah, ilisema wanachama wa kundi hilo walikamatwa Januari 12, siku moja kabla, “walikuwa na nia ya kufanya operesheni za uasi”. Taarifa ya DGRM haikutoa maelezo zaidi kuhusu “operesheni”.