Burundi imetoa hati ya kimataifa ya kukamatwa kimataifa kwa mwanasiasa wa upinzani aliye uhamishoni Alexis Sinduhije, ikimtuhumu kwa kuongoza kundi linalohusika na vitendo kadhaa vya kigaidi mwanasheria mkuu wa nchi hiyo alisema.
Tangazo la Sylvestre Nyandwi Jumatano usiku lilitolewa baada ya msururu wa mashambulizi katika taifa hilo la Afrika Mashariki katika siku za karibuni, ambapo watu sita walipoteza maisha na zaidi ya mia moja kujeruhiwa.
Lakini hati hiyo inahusiana na mashambulizi ya awali, pamoja na milipuko ya mabomu na uvamizi ambapo dazeni ya watu waliuawa na kujeruhi wengine zaidi ya 100 tangu mwanzoni mwa mwaka 2020, mwanasheria mkuu alisema.
Uchunguzi uliofanywa tayari umebaini kuwa vitendo hivi vimefanywa na kundi la magaidi waklongozwa na Alexis Sinduhije, alidai.
Chini ya sheria ya kitaifa na kimataifa, vitendo hivi ni vitendo vya ugaidi, na pia uhalifu dhidi ya ubinadamu. "
Rais wa chama cha upinzani cha Movement for Solidarity and Development (MSD), Alexis Sinduhije anaishi uhamishoni nchini Ubelgiji.