Burundi yadai uhusiano wake Rwanda hautovunjika

Rais wa Burundi Pierre Nkurunzinza katika picha

Kauli hiyo imetolewa na msemaji wa serikali ya Burundi siku moja baada ya Desire Nyaruhirira aliyekuwa mshahuri mkuu kwenye ubalozi wa Rwanda jijini Bujumbura kufukuzwa na serikali ya Burundi.

Hatua ya Burundi ya kumufukuza kwenye ardhi yake mwanadiplomasia wa Rwanda haitazorotesha kamwe uhusiano wa Burundi na Rwanda.

Kauli hiyo imetolewa na msemaji wa serikali ya Burundi siku moja baada ya Desire Nyaruhirira aliyekuwa mshahuri mkuu kwenye ubalozi wa Rwanda jijini Bujumbura kufukuzwa na serikali ya Burundi.

Bwana Phillippe Nzobonariba amesema kuwa hatua hiyo imechukuliwa dhidi ya mtu kutokana na mwenendo wake usiofaa sio kwa taifa la Rwanda.Hata hivyo nchi hizo zimekuwa zikilaumiana, Burundi ikilaumu Rwanda kuwapa hifadhi na kuwasaidia wanaopanga njama ya kupigana dhidi ya serikali ya Burundi huku Rwanda upande wake ikituhumu Burundi kuwahifadhi waasi wa kihutu wa FDRL waliofanya mauwaji ya kimbari nchini Rwanda mwaka wa 1994.

Msemaji wa serikali ya Burundi amesema kwamba ni vyema watu waelewe kwamba hatua ya kumfukuza mwanadiplomasia huyo kutoka Rwanda aliyehudumu katika ubalozi wa Rwanda nchini Burundi kwa zaidi ya miaka kumi ilichukuliwa ili kukinga uhusiano wa kati ya mataifa hayo mawili yanayopakana usizorote kutokana na mwenendo wa mtu huyo ambaye anasema ulikiuka mwenendo na kanuni za kidiplomasia . Mwandishi wetu Haidalaha Hakizimana anatupasha zaidi kutoka Bujumbura.

Your browser doesn’t support HTML5

Burundi yadai uhusiano wake na Rwanda hautovunjika