Bunge la Marekani limekubaliana dola trilioni 1.6 kuepuka kufunga serikali kuu

Spika wa Baraza la Wawakilishi Marekani, Mike Johnson akizungumza mjini Washington

Takwimu za juu ni pamoja na dola bilioni 886 kwa ajili ya ulinzi na dola bilioni 704 kwa matumizi yasiyo ya ulinzi, kulingana na spika Mike Johnson.

Viongozi wa juu wa bunge la Marekani, Jumapili walikubaliana juu ya dola trilioni 1.6 katika kipaumbele cha matumizi ya serikali kuu kwa mwaka wa fedha 2024 katika makubaliano yanayolenga kuepusha kufungwa kwa sehemu ya taasisi za serikali baadaye mwezi huu, Spika wa Baraza la Wawakilishi la Marekani, Mike Johnson alisema.

Takwimu za juu ni pamoja na dola bilioni 886 kwa ajili ya ulinzi na dola bilioni 704 kwa matumizi yasiyo ya ulinzi, Johnson, m-Republican alisema katika barua yake kwa wabunge Jumapili. Sehemu ya ulinzi tayari ilikwisha sainiwa kuwa sheria na Rais Joe Biden mwezi uliopita kupitia muswaada wa matumizi ya ulinzi.

Kiongozi wa Democratic katika baraza la wawakilishi Hakeem Jeffries.

Fedha hizo zisizo za ulinzi zitalinda vipaumbele muhimu vya ndani kama vile mafao ya wastaafu, huduma za afya na msaada wa lishe, kutokana na punguzo la bajeti lililofanywa na baadhi ya Wa-Republican, Kiongozi wa wademocrat walio wengi katika Baraza la Seneti Chuck Schumer na kiongozi wa chama cha Democratic katika baraza la wawakilishi Hakeem Jeffries wamesema katika taarifa ya pamoja.

Taarifa yao iliweka matumizi yasiyo ya ulinzi kwa dola bilioni 772.7 karibu dola bilioni 69 zaidi ya ilivyoelezwa na Johnson. Mshauri wa chama cha Democratic amesema fedha hizo za ziada ni “mabadiliko madogo kufikia lengo”.