Kundi la wanamgambo la Boko Haram limeshambulia kusinimashariki mwa Niger na kuuwa wanajeshi 34 na kujeruhi wengine 67.
Shambulizi hilo lilizuka jumamosi mchana wakati ambapo maelfu ya wapiganaji wa Boko Haram walipoelekea Bosso na kuchukua magari yaliyokuwa na silaha nzito.
Wapiganaji hao wa Boko Haram walitumia silaha nzito hata kabla ya kuingia kwenye mji huo .
Wanajeshi wa Nigeria walilazimishwa kuondoka katika kambi yao kilomita 20 mbali na mji ili kujiandaa kusaidia.
Vikosi vya ulinzi na usalama baadae vilichukua tena udhibiti wa mji . wanajeshi wawili wa Nigeria ni miongoni mwa waliouwawa.
Washambuliaji waliweza kuchukua magari yenye silaha nzito na vifaa vingine . hivi sasa watu bado wanaishi katika hali ya wasiwasi kufuatia shambulizi hilo, ingawa mji uko kimya.