Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken, amesema Israel kufanya kazi na majirani wa Kiarabu katika Mashariki ya Kati ili kufungua njia kwa taifa la Palestina ni njia bora zaidi ya kuitenga Iran.
Kabla ya kuondoka Cairo, ambako alifanya mazungumzo na Rais wa Misri, Abdel Fattah el-Sissi, Blinken alisema “Kuna njia ambayo inaleta mahitaji na matarajio ya Israel ya mingiliano katika eneo hilo pamoja na usalama wa kweli, pamoja na utashi wa Palestina kwa taifa lao wenyewe.
“Hiyo ndiyo njia bora Zaidi, muingiliano huu, usalama, taifa la Palestina kulitenganisha na kuitenga Iran na aina ya hatua inazochukua kupitia washirika wake,” Blinken alisema.
“Nadhani maono hayo yapo wazi lakini kwa sisi kusonga mbele katika hilo, na jambo hilo liweze kuanza, mgogoro wa Gaza lazima umalizike. Hii ni muhimu sana.”
Wakati huo huo, Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amepinga vikali suluhisho la mataifa mawili.