Rais wa FIFA ajiuzulu

Rais wa FIFA Sepp Blatter

Rais wa Shirikisho la Kandanda Duniani Sepp Blatter amejiuzulu wadhifa huo muda mfupi uliopita. Akitokea mbele ya waandishi wa habari Jumanne Juni 2 Blatter alisema kwa masikitiko makubwa anajizulu wadhifa huo.

Blatter amekuwa akikabiliwa na shinikizo kubwa kujiuzulu tangu maafisa kadha wa FIFA kutiwa nguvuni kwa shutuma za rushwa wiki iliyopita.

Kiongozi huyo wa FIFA aliyechaguliwa kwa mara ya kwanza 1998 na kuchaguliwa tena kwa mhula wake wa tano tarehe 29 JUne 2015, amesema ataitisha mkutano wa dharura wa baraza kuu la shirikisho kumchagua rais atakae chukua nafasi yake.