Biden azindua mpango wa matumizi ya serikali wenye dhamani ya dola trilioni 6.8

Rais wa Marekani Joe Biden

Rais wa Marekani Joe Biden Alhamisi amezindua mpango wa matumizi ya serikali wenye thamani ya dola trilioni 6.8 kwa mwaka 2024, huku akitangaza sera kadhaa mpya ikiwemo kuongeza kodi kwa mashirika makubwa pamoja watu matajiri.

Hata hivyo wapinzani kutoka chama cha Republikan haraka walisema kwamba pendekezo hilo huenda lisipitishwe katika Bunge. Biden ambaye ni mdemokrat anayeongoza muhula wa kwanza, na anayelenga kuwania urais kwa muhula wa pili mwaka ujao anapendekeza fedha zaidi za matumizi ili kukabiliana na ushawishi wa China, kiuchumi na kijeshi, matumizi kwenye mfumo wa afya kwa wamarekani wote vijana na wazee, mikakati mipya kwa masomo na kuongeza wafanyakazi kwenye idara ya kitaifa ya hifadhi ya mazingira.

China ndiye mshindani pekee wa Marekani mwenye uwezo wa kubuni mfumo mpya wa kiuchumi ulimwenguni, wakati taifa hilo likiwa na uwezo wa kiuchumi, kidiplomasia, kijeshi na kiteknolojia kufanya hivyo. Mpango wa Biden umekuja wakati kuna mgawanyiko mkubwa bungeni kuhusu namna ya kuongeza kiwango cha kukopa cha serikali kutoka dola trilioni 31.4 kikiwa kiwango ambacho serikali inaweza kukopa ili kulipia madeni