“Kwa muda wote wanaotumia kunishambulia pamoja na mipango yangu, wenyewe hawasemi wanachotaka kufanya,” Biden alisema wakati akitoa hotuba kwenye chuo cha Prince George’s Community College, mjini Largo, jimbo la Maryland.
Amesema kwamba mpango wa Warepablikan umevuka mipaka kwa viwango ambavyo Marekani haijawahi kushuhudia.
Biden pia alikashifu mpango wa Repablikan wa kupunguza kodi kwa matajiri pamoja na makampuni makubwa, pamoja na kupunguza fedha kwenye program kama za malipo ya uzeeni na bima za afya za Madicare na Medicaid.
Aliongeza kusema kwamba mamilioni ya Wamarekani huenda wakapoteza bima zao za afya chini ya mpango wa kifedha wa wa-Repablikan.