Benki kuu ya Uganda inatafakari kutoa sarafu ya kidigitali, na haijapiga marufuku sarafu ya kimtandao “cryptocurrencies”.
Benki kuu ya Uganda inatafakari kutoa sarafu ya kidigitali, na haijapiga marufuku sarafu ya kimtandao “cryptocurrencies” lakini ina wasiwasi kuhusu madhara ya kiteknolojia ikiwemo kumlinda mteja, na uhalifu wa kifedha amesema afisa mwandamizi wa benki kuu ya Uganda, Ijumaa.
Benki hiyo kwa sasa inafanya utafiti wa awali kufahamu kuruhusiwa ama la kwa sarafu za kimtandao alisema Andrew Kaware mkurugenzi wa malipo ya taifa.
Alisema hayo kwa shirika la habari la Reuters, na kwamba wanaendelea kufanya utafiti wa sera ambazo zitastahili. Serikali za Afrika zimeshughulikia sarafu ya kimtandao tofauti-tofauti kulingana na mazingira yake.