Benki kuu ya Kenya imepunguza makadirio yake ya ukuaji wa uchumi kwa mwaka huu hadi asilimia 5.5, maelezo ya gavana wa benki hiyo Patrick Njoroge yalibainisha hivi leo Jumatano.
Benki hiyo ilisema mwezi Machi kwamba uchumi ungepanuka kwa asilimia 5.8. Njoroge hakuelezea utabiri huo mpya. Uchumi ulipanuka kwa asilimia 4.8 mwaka jana,ikiwa ni chini ya kasi ya ukuaji wa mwaka 2021 uliolemewa na mdororo katika sekta ya kilimo.
Njoroge, ambaye atauacha wadhifa huo katikati ya mwezi ujao baada ya miaka minane, alisema alitarajia sekta ya kilimo itaimarika kutokana na athari za kudorora za mwaka jana na mvua za kutosha zimenyesha kote nchini.
Kilimo kinachangia pato kubwa la uchumi katika taifa hilo. Utalii, ni sekta nyingine muhimu inaripoti mustakabali mzuri wa siku zijazo gavana alisema, akiashiria utendaji mzuri katika miezi ijayo.