Baraza la Usalama la UM lapiga kura kusitisha kazi za Ofisi ya kulinda amani Mali

Wanachama wa kikosi cha MINUSMA wakivuta gari lao lililokwama wakati wa msafara wa vifaa kutoka Gao hadi Kidal. REUTERS.

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilipiga kura kwa kauli moja  Ijumaa kusitisha kazi za Ofisi ya kulinda amani iliyodumu kwa muongo mmoja

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilipiga kura kwa kauli moja Ijumaa kusitisha kazi za Ofisi ya kulinda amani iliyodumu kwa muongo mmoja nchini Mali baada ya utawala wa kijeshi wa nchi hiyo ya Afrika Magharibi kuwataka ghafla wanajeshi 13,000 wiki mbili zilizopita kuondoka mara moja.

Kumalizika kwa operesheni hiyo, inayojulikana kama MINUSMA, kunafuatia miaka mingi ya mivutano na vikwazo vya serikali ambavyo vimesababisha operesheni za ulinzi wa amani za anga na ardhini tangu Mali ilipoungana na kundi la mamluki la Wagner la Russia mwaka 2021.

Baraza hilo lenye wanachama 15 lilipitisha azimio lililoandaliwa na Ufaransa likitaka ujumbe huo uanze siku ya Jumamosi kusitishwa kwa shughuli zake, uhamisho wa majukumu yake, pamoja na kupunguzwa kwa taratibu na salama kwa wafanyakazi wake, kwa lengo la kukamilisha mchakato huu kufikia Desemba 31, 2023.