Ban asisitiza suluhisho la kisiasa kwa mzozo wa mashariki ya Kongo

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon akutana na rais Joseph Kabila kando ya mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Kii Moon asisitiza haja ya kumaliza maafaa yanayosababishwa na mzozo wa mashariki ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Akizungumza kwenye mkutano wa viongozi kutoka karibu nchi 30 kando ya mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Matiafa mjini New York siku ya Alhamisi, Bw Ban alitoa wito wa kupatikana suluhisho la haraka na kwa njia ya amani kupitia msinigi ya majadiliano.

"Hakuna suluhisho la kijeshi kwa mzozo huo. Nilazima tutafakati kuweza kupata mapendekezo thabit katika kumaliza mzozo kwa njia ya amani."

Your browser doesn’t support HTML5

Mkutano wa viongozi juu ya DRC




Rais Paul Kagame wa Rwanda aliyehudhuria mkutano anassema amekanusha vikali tuhuma kwamba nchi yake inawasaidia waasi wa M23. Baada ya mkutano rais Kagame alisema mzozo huo hauwezi kutanzuliwa ikiwa jumuia ya Kimataifa itaendelea eleza mzozo huo kwa njia ya upotofu.

Kiongozi huyo alondoka kwenye ukumbi wa mkutano kabla ya kumalizika mazungumzo ambapo waloshiriki walilaani vikali msaada wowote wa kigeni kwa kundi la M23, na makundi mengine ya waasi yanayosababisha vurugu huko mashariki ya Kongo.