Balozi wa marekani nchini Nigeria ametoa mtazamo wake kuhusu uchaguzi

Mary Beth Leonard, balozi wa Marekani nchini Nigeria

Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi ya Nigeria (INEC) ilimtangaza Bola Tinubu kuwa rais ajaye wa Nigeria. Mwenyekiti wa INEC Mahmood Yakubu amesema Tinubu, mgombea wa chama tawala cha All Progressives Congress alipata karibu kura milioni 8.8 na kuwashinda wapinzani wake

Balozi wa Marekani nchini Nigeria amekiri katika taarifa Jumapili kwamba kufuatia uchaguzi wa karibuni katika taifa hilo la Afrika "kuna Wa-Nigeria wengi wenye hasira na waliokatishwa tamaa pamoja na wengi wanaosherehekea ushindi." Mary Beth Leonard alihimiza kwamba "mchakato uliowekwa kisheria wa kutatua changamoto za uchaguzi uruhusiwe kuchukua mkondo wake."

"Kadri inavyoweza kuwa hairidhishi kumaliza mchakato wa uchaguzi katika chumba cha mahakama, katika demokrasia ya kikatiba iliyowekwa na utawala wa sheria, "Leonard alisema, "hapo ndipo migogoro ya uchaguzi inaweza kuhitimishwa ipasavyo."

Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi ya Nigeria (INEC) ilimtangaza Bola Ahmed Tinubu kuwa rais ajaye wa Nigeria. Mwenyekiti wa INEC Mahmood Yakubu amesema Tinubu, mgombea wa chama tawala cha All Progressives Congress alipata karibu kura milioni 8.8 na kushinda kinyang'anyiro kikali zaidi tangu Nigeria iwe taifa la kidemokrasia.

Viongozi wa upinzani wameutaja uchaguzi huo kuwa wa "kihuni" na wameahidi kwenda mahakamani kupinga matokeo hayo.