Hilo linajiri kabla ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu Julai 23, wakati kukiwa na madai ya tishio na ukandamizaji kutoka kwa serikali, hali inayotoa changamoto kubwa kwa viongozi wa upinzani waliobaki. Mei serikali iliondoa chama kikuu cha upinzani cha Candlelight kwenye kushiriki uchaguzi huo, hatua iliyopelekea wanachama wake kuhama kwa haraka.
Hata kabla ya hatua hiyo kuchukuliwa, wanasiasa walikuwa wakiondoka kwenye upinzani kwa wingi, wakati waziri mkuu Hun Sen akidaiwa kuandama baadhi yao na kesi za mahakama, ukamataji pamoja na kupigwa katika miezi ya karibuni.
Msemaji wa chama cha Candlelight Kimsour Phririth, anakisia kwamba asilimia 10 – 15 ya viongozi wa chama hicho wameondoka. Msemaji wa chama tawala Sok Eysan kwa upande wake amesema kwamba maelfu ya wafuasi wa upinzani pamoja na maafisa yamekuwa wakijiunga na chama hicho ndani ya mwaka mmoja uliopita bila kutoa ushahidi wowote.