Umoja wa Afrika (AU) umeelezea wasiwasi mkubwa juu ya kuzuka kwa mapigano makali nchini Libya wiki hii na kutoa wito wa kusitishwa mara moja kwa uhasama na kuanza juhudi za kutafuta maridhiano.
Watu 55 wameuawa na wengine 146 kujeruhiwa katika mapigano mabaya kutokea katika kipindi cha mwaka mmoja katika mji mkuu Tripoli ambayo yalizuka Jumatatu usiku, vyombo vya habari vya Libya vimeripoti.
Mkuu wa Tume ya Umoja wa Afrika, Moussa Faki Mahamat anafuatilia wasiwasi huo kwa karibu kuhusu maendeleo ya hali ya usalama mjini Tripoli ambayo yamesababisha vifo vya watu wengi na wengine kadhaa kujeruhiwa, ilisema taarifa ya taasisi hiyo ya Afrika.
Faki anawasihi wadau na watendaji wote wa kijeshi, kisiasa na kijamii kukomesha mara moja uhasama huo na kuwakumbusha wadau wote umuhimu wa kufanya juhudi zinazoendelea kuelekea maridhiano ya kitaifa, ilisema taarifa.
Pia ameonya kuwa hakuna suluhisho la kijeshi kwa mzozo wa Libya na kwamba umoja wa Libya, amani, utulivu na hadhi ya kihistoria ya kimataifa vinaweza tu kupatikana kwa njia za amani.