Baadhi ya matokeo yalionyesha muungano wa Liberal National wa Morrison uliadhibiwa na wapiga kura katika eneo la Australia Magharibi na viti vya mijini kwa matajiri.
Usiku wa leo, nimezungumza na Kiongozi wa Upinzani na Waziri Mkuu ajaye, Anthony Albanese. Na nimempongeza kwa ushindi wake wa uchaguzi jioni hii," Morrison alisema, akijiuzulu kama kiongozi wa chama chake.
Labour walikuwa bado hawajafikia viti 76 kati ya 151 vya bunge vinavyohitajika kuunda serikali peke yao. Matokeo ya mwisho yanaweza kuchukua muda kwani bado wanaendelea kuhesabu idadi ya kura nyingi zilizopigwa kwa njia ya posta.