Amri ya kiutendaji inayoelekeza uchunguzi huo iko bado katika mipango lakini inaweza kuchukua wiki kadhaa baadae kutekelezwa, maafisa wawili wa ngazi za juu Ikulu ya Marekani wamesema Ijumaa.
Japokuwa Trump aliwaamrisha wafanyakazi kuanza mara moja mradi huo wiki iliyopita, hajalizungumzia suala hilo siku za karibuni, kwa mujibu wa watu wengine wawili ambao wana mawasiliano ya karibu na rais.
Watu wote hao walitaka majina yao yasitajwe ilikuweza kuzungumzia mambo haya binafsi.
Hali halisi ya uchunguzi
Alipoulizwa kuhusu mahali ilipofikia kadhia hii, Msemaji wa White House Lindsay Walters amesema: Mimi sina habari yeyote mpya hivi sasa.”
Ucheleweshaji huu usio na kikomo wa taarifa hizi umekuja wakati baadhi ya washauri wa Trump walipomrai kuwa aachane na uchunguzi huu, kwani unamzuilia kushughulika mambo muhimu zaidi.
Utaratibu wa kupiga kura
Hakuna ushahidi juu ya wizi mkubwa wa kura katika uchaguzi mkuu wa Novemba. Trump alishinda kura za wajumbe “Electoral College” lakini alipoteza kura za umaarufu kwa idadi ya kura milioni 2.9 ambazo zilichukuliwa na mgombea wa Demokratik Hillary Clinton.