Ajali ya kwanza ilitokea Julai mosi, mwaka huu katika eneo la mteremko wa Mlima Mbalizi iliyotokana na magari manne kugongana na kusababisha vifo vya watu 20 na kujeruhi 45.
Wakati huo huo Waziri wa Mambo ya Ndani Kangi Lugola amesema kuwa Leopold Fungu ambaye ni Mrakibu wa Polisi amemshusha cheo hicho na kubaki na nyota tatu kutokana na ajali za Mbeya. | |
Vyanzo vya habari nchini Tanzania vimeripoti kuwa alisema wakati akiapishwa na Rais Magufuli alimwambia kuwa anachukizwa na matukio ya ajali hasa ile ya Mbeya iliyosababisha vifo vya watu 20. |
|
Alisema baada ya kuapishwa alikwenda Mbeya na ndipo alipolazimika kuvunja mabaraza ya Kamati ya Usalama barabarani |
|
“Nilipokuwa Mbeya nilitaka kujua idadi ya wajumbe walioko kwenye kamati hii ya usalama barabarani, lakini walishindwa kujua idadi wala majina ndiyo nikatangaza kuivunja,” alisema
Akithibitisha kutokea kwa ajali ya pili, Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Mussa Taibu, alisema Jumapili ajali hiyo imethibitishwa.
Alisema katika ajali hiyo watu watano akiwamo Ofisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Mbeya, Izack Nchembi, walipoteza maisha papo hapo na mmoja kujeruhiwa na chanzo cha ajali hiyo ni kufeli kwa breki ya lori lililokuwa likitokea Mpaka wa Kasumulu.
“Watatu walikuwa katika lori lililobeba sukari ambao mmoja ni mtumishi wa TRA, dereva na utingo, wengine wawili walikuwa katika Noah,” alisema.
Kutokea mfululizo kwa matukio hayo ya ajali, kumezua hofu kwa baadhi ya wakazi wa Mbeya na wengi wamehoji iweje mazingira yake yafanane.
“Ukiangalia ajali ya Mbalizi, chanzo tunaambiwa ni breki, ajali imehusisha gari nne, gari ndogo moja ilifunikwa na kontena na hii ya leo (juzi) tunaambiwa ni kufeli kwa breki, gari nne na moja ndogo imefunikwa na kontena, hapa wananchi tunapatwa na hofu,” alisema Ismail Mwambapa, ambaye ni mkazi wa Uyole.