Shirika hilo limeongeza kusema kuwa maambukizi ya sasa yanaenea kwa haraka kuliko wimbi la pili lililoanza mwanzoni mwa mwaka. WHO linasema kuwa hali hiyo huenda imesababishwa na kutozingatia kanuni zilizo wekwa, ongezeko la mikusanyiko pamoja na aina mpya ya virusi vya corona.
Aina mpya ya virusi kwa jina delta,vilivyo gunduliwa kwa mara ya kwanza nchini India, sasa vimeripotiwa kwenye mataifa 14. Ukosefu wa chanjo pia unasemekana kuchangia hali hiyo, WHO likisema kuwa mataifa 18 tayari yamemaliza karibu asilimia 80 ya chanjo zake huku mataifa manane yakiishiwa kabisa.
Kufikia sasa ni asilimia 1 tu ya watu barani Afrika waliopokea chanjo dhidi ya corona kwa mujibu wa WHO. Mkuu wa kituo cha Afrika cha kudhibiti na kuzuia magonjwa John Nkengasong, amesema kuwa wimbi la sasa limekuja kwa kishindo kulivyo ilivyo tarajiwa.