Polisi Afrika Kusini wajitetea kwa kuuwa wachimba migodi

  • Esther Githui-Ewart

Mwanamke alia baada ya polisi kuuwa wachimba migodi katika mgodi wa Lonmin Platinum Afrika Kusini, Agosti 17, 2012.

Mkuu wa polisi wa Afrika Kusini Riah Phiyenga amesema vikosi vyake viliwafyatulia risasi wafanyakazi wachimba madini wanaogoma kwa ajili ya kujilinda katika ghasia zilizosababisha vifo vya watu 34 na 78 kujeruhiwa.

Kamanda Phiyega amesema polisi walitumia nguvu kupindukia kujilinda wenyewe baada ya kushambuliwa na wachimba migodi wanaogoma waliokuwa na silaha hatari siku ya Alhamis. Kampuni ya mgodi wa Lonmin PLC karibu na Johannesburg, wanakofanya kazi wengi wa wanaogoma imekiri pia kwamba baadhi ya wafanyakazi hao walikuwa na silaha.

Akizungumza na Sauti ya Amerika kutoka Johanesburg mwandishi habari Egbert Mkoko anasema mzozo ulianza wiki moja iliyopita baada ya wachimba madini elfu tatu walipoanza mgomo kudai nyongeza kwa karibu asili mia 300 na hali bora za kazi.

Your browser doesn’t support HTML5

Mahojiano na Egbert Mkoko


Rais Jacob Zuma alifupisha safari yake ya Maputo na kurudi nyumbani Ijumaa akisema katika taarifa kwamba ameshtushwa na kuchukizwa na kile alichokieleza kuwa ghasia zisizo na maana. Hakusema anayewajibika lakini alivihimiza vyama vya wafanyakazi kufanyakazi na serikali kutanzua hali hiyo.

Polisi wa Afrika Kusini wauwa wachimba migodi 34


Msemaji wa chama cha kitaifa cha wachimba madini Lesina Seshoka anasema sehemu ya mvutano huo imechochewa na uwamuzi wa wafanyakazi kuanza mgomo bila ya kupata uungaji mkono wa chama cha wafanyakazi.