Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, kutumwa kwa kikosi hicho cha jeshi la kitaifa cha SANDF kinatarajiwa kutumia takriban dola milioni 26 za kimarekani ambazo ni sawa na randi milioni 492 za Afrika Kusini, wakati kikilenga kuhakikisha utekelezaje wa sheria chini ya mpango wa Operation Prosper, msemaji wa Ramaphosa, Vincent Magwenya amesema kupitia taarifa.
Jeshi la Afrika Kusini lilitumika 2019 kwenye jimbo la Western Cape ili kupambana na ghasia za magenge, kwenye operesheni sawa na hiyo. Taarifa zimeongeza kwamba jeshi litashirikiana na idara ya polisi ya Afrika Kusini katika kukabiliana na uchimbaji haramu wa madini kwenye majimbo yote kuanzia mwisho wa mwezi uliopita hadi Aprili 28 mwaka ujao.
Baraza la madini la Afrika Kusini limesema kwamba uchimbaji haramu nchini humo hufanyika kwenye migodi iliyoachwa pamoja na ya sasa, suala ambalo linazuia wawekezaji kuingia nchini.