Vijana wa Afrika wahamasishwa kujiunga katika kilimo

Mkulima wa mihogo

Ripoti inaeleza kwamba hapa Marekani, na nchi nyenginezo, pale vijana wanapoingia tu vyuo vikuu, wanaanza mfumo wa kujitayarisha katika kukopa na kulipa mikopo yao.

Ripoti ilotolewa hivi karibuni inaonya kuwa bara la Africa halitoweza kupunguza tatizo sugu la upungufu wa chakula na ukosefu wa ajira, hadi pale vijana watakapojihusisha Zaidi katika kilimo.

Ripoti hiyo ilopewa jina la “Youth in Agriculture in Sub Saharan Africa” yaani vijana katika kilimo katika nchi za kusini mwa jangwa la Sahara, iliandaliwa na muungano unoongozwa na waafrika unaojulikana kama Alliance for Green Revolution au kwa kifupi AGRA, kwa kuzingatia kuwaweka wakulima katikati ya uchumi unaokuwa wa bara hilo.

Davis Sarfo Ameyaw, mhariri mkuu wa ripoti hiyo na mkuu wa mikakati ya AGRA, anasema utafiti huo umegundua kuwa vijana wengi wa Africa, hususan wale walio soma, wanachukulia kufanya kazi kwenye ya kilimo ni ngumu na yakuchokesha.

Ripoti imegundua kwamaba ni asli mia 9 tu ya vijana huko Ethiopia wanasema wanapanga kufanya kazi katika sekta ya kilimo. Kwa upande mwengine, vijana wengi wa Nigeria wanatazamia ajira katika kilimo kuwa ni jambo zuri. Hili huwenda kuwa ni kwa ajili ya juhudi za taifa hilo kufanya kilimo kuwa nyanja yenye kivituo kwa vijana kuweza kufwata.

Ameyaw alitaja changamoto kadha kubwa ambazo zitawakabili wakulima hao watarajiwa. Kwanza ni kupatikana kwa ardhi. Anasema serikali za Africa zinapaswa kubuni soko la ardhi ili kuwaleta pamoja wanunuzi na wauzaji na kutowa maelezo juu ya ardhi zinazouzwa.

Kizingiti kingine kikuu ni kuwawezesha vijana kupata mikopo ambayo itawaruhusu kununuwa ardhi.

Your browser doesn’t support HTML5

AFRICA YOUTH UNEMPLOYMENT

Anasema wameshuhudia kuwa takriban asli mia 90 ya vijana chini ya umri wa maiak 35 wameweza kupata mikopo, lakini sio kutoka taasisi za fedha. Mikopo hiyo inatoka kwa aidha baba au ama au marafiki au familia zao.

Bw Ameyaw anasema kubuniwa kwa mfumo wa ukopeshaji ni chanzo muhimu katika kuwafanya vijana kupenda kilimo. Anasema kupatikana kwa fedha kutawasaidia kubuni nafasi za kazi katika nyanja za kilimo.

Anasema kile kinachofanya tatizo hilo kuwa cha dharura Zaidi , ni kwamba mamillioni ya wakulima barani humo wanategemea bidhaa kutoka nje kulisha familia zao. Bidhaa hizo ghali ni mzigo mkubwa kwa fedha za serikali na hazifanyi lolote kushughulikia ukosefu wa ajira.

Wakati huo huo, bara la Africa lina idadi kubwa inayoongezeka ya vijana, ambao wanaweza kuwa na manufaa katika nyanja ya kilimo.

Ameyaw anasema, bara Africa linakabiliwa na matatizo mawili makuu, nayo ni ukosefu wa usalama wa chakula na ukosefu wa ajira. Madhumuni ya ripoti hiyo ni kwamba iwapo serikali na watunga sera, washika dau wanaweza kutatuwa matatizo hayo ambayo bara hilo linakabiliwa nayo, basi tutaweza kutatuwa ukosefu wa usalama wa chakula, ukosefu wa ajira na matatizo ya umasikini yanayokabiliwa barani humo.