Netanyahu asema wanaahirisha kwa muda kuidhinisha makubaliano ya Gaza

  • VOA Swahili

Your browser doesn’t support HTML5

Mashambulio ya Israel yamendelea kufanyika katika ukanda wa Gaza Alhamisi licha ya kutangazwa makubaliano ya kusitisha mapigano na kuachiliwa kwa mateka na wafungwa wa Kipalestina.

Wizara ya afya ya Gaza imesema Alhamisi kwamba karibu watu 72 wameuliwa usiku wa Jumatano kuamkia Alhamisi kutokana na mashambulio makali yaliyofanywa na jeshi la Israel huko Gaza muda mchache baada ya wakazi wa kanda hiyo kusherehekea tangazo la makubaliano ya kusitisha mapigano.

Na ofisi ya Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu imetangaza kwamba mkutano wa baraza la mawaziri ulopangwa kuidhinisha makubaliano hayo umeahirishwa, ikikituhumu kundi la Hamas kupinga sehemu ya makubaliano, katika jaribio la kupata ridhaa zaidi.

Netanyahu amesema tatizo la dakika ya mwisho kutoka kwa Hamas linazuia Israel kuidhinisha mkataba huo ulokua ukisubiriwa kwa muda mrefu. Ofisi yake haikutoa maelezo zaidi.