Makundi ya haki yanafurahia mahakama maalum ya uhalifu wa Gambia

Your browser doesn’t support HTML5

Makundi kadhaa ya kutetea haki za binadam nchini Gambia yame karibisha uwamuzi wa Jumuia ya Uchumi ya nchi za Afrika Magharibi ECOWAS kwa kuunga mkono kuundwa kwa mahakama maalum kuhukumu uhalifu ulotendwa wakati wa utawala wa kimabavu wa Yahya Jammeh.

Taarifa ya ECOWAS inaeleza kwamba mahakama hiyo itahakikisha haki na uwajibikaji kutokana na ukiukaji mkubwa wa haki za binadam ulolfanyika kati ya 1994 hadi July 2017 unatendeka.

Taarifa hiyo ya ECOWAS iliyotolewa baada ya viongozi kukutana Jumapili mjini Abuja, Nigeria inaeleza kwmba hii ni mara ya kwanza kwa Jumuia hiyo kushirikiana na nchi mwanachama kuunda mahakama maalum kama hiyo.

Utawala wa miaka 22 was Jammeh uligubikwa na idadi kubwa ya ukiukaji wa haki za binadam na utumiaji mbaya wa fedha za taifa kwa ajili ya matumizi binafsi ya kiongozi huyo aliyejihisi mkubwa kuliko mtu yeyote yule.