Rais wa Tume ya Ulaya Ursula Von der Leyen alisema Ijumaa juhudi za kupata misaada kuingia Gaza kupitia bandari ya Cyprus zilielezwa Alhamisi usiku na Rais Joe Biden katika hotuba yake ya Hali ya Kitaifa kwamba itaanza kufanya kazi ifikapo Jumapili, au mapema zaidi ya hapo.
Akizungumza katika mkutano wa pamoja na waandishi wa habari leo Ijumaa na Rais wa Cyprus Nikos Christodoulides huko Cyprus, Von der Leyen alisema ukanda huo ulikaribia kufunguliwa, na unaweza kuanza kufanya kazi Jumapili, na pengine ikawa mapema Jumamosi, ambapo mpango wa majaribio wa awali umeanza Ijumaa.
Katika hotuba yake ya kila mwaka ya Hali ya Taifa kwa Bunge la Congress, Rais Biden alisema jeshi la Marekani litaongoza kazi za dharura za kujenga gati ya muda katika Bahari ya Mediterania kwenye pwani ya Gaza ambayo inaweza kupokea shehena kubwa za chakula, dawa, maji na makazi ya muda.