Rais wa Ushelsheli atangaza hali ya dharura kufuatia mafuriko na mlipuko

  • VOA Swahili

Rais Wavel Ramkalawan akihutubia mkutano wa COP28 mjini Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu

Rais Wavel Ramkalawan wa Ushelsheli ametangaza hali ya tahadhari Alhamisi, akiwaamuru raia wote isipokuwa wafanyakazi muhimu kubaki nyumbani, baada ya mlipuko katika duka moja la vilipuzi na mafuriko kutokana na mvua kubwa.

Taarifa ya Ikulu mjini Victoria, imetolewa kufuatia mlipuko mkubwa kwenye duka la vilipuzi la CCCL katika mtaa wa viwanda kwenye kisiwa kikuu cha Mahe na kusababisha uharibifu mkubwa na kumsababisha rais kutangaza hali ya dharura.

Mlipuko huo umetokwa pia wakati mvua nyingi kusababisha mafuriko yaliyowauwa watu watatu na Rais Ramkalawan kutangaza Disemba 7 kua siku ya dharura visiwani humo na uharibifu pia mkubwa uliosababishwa na mafuriko kutokana na mvua nyingi, Rais ametangaza hali ya dharura kwa leo tarehe 7 Desemba.

Jengo lililoharibiwa na mlipuko kwenye ghala ya vilipuzi kwenye mtaa wa viwanda mjini Mahe, Ushelsheli. Disemba 7, 2023.

Shule zote zimefungwa na wafanyakazi wa idara muhimu tu na watu wanaosafiri ndio wanaruhusiwa kutembea kwa nafasi. Hii ni kuruhusu idara za dharura kutekeleza kazi muhimu taarifa hiyo iliongeza.

Ushelsheli ambayo ni kituo muhimu cha utali ina jumla ya visiwa 115 na wakazi wapatao 100,000 kwenye bahari ya Hindi, mashariki mwa Afrika.